Transcription of SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HOTUBA YA WAZIRI …
1 1 SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI JUNE 2017 i YALIYOMO A. UTANGULIZI .. 1 B. HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO .. 7 C. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2016/17 .. 8 Mapato .. 8 Mapato ya Ndani .. 8 Mapato ya Nje .. 9 MATUMIZI .. 9 D. UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA KIPINDI CHA MIEZI TISA (JULAI 2016 - MACHI 2017): .. 10 MAPATO .. 10 E. MFUKO WA MIUNDOMBINU (INFRASTRUCTURE FUND) .. 16 F. DENI LA TAIFA: .. 18 G. UTEKELEZAJI WA HATUA ZA KUIMARISHA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017.
2 19 H. MATARAJIO HADI JUNI 2017 .. 21 MAPATO .. 21 MATUMIZI .. 22 I. MAREKEBISHO YA MISHAHARA, 2016/2017 .. 23 J. MWELEKEO WA BAJETI YA 2017/18 .. 28 K. VIPAUMBELE VYA KITAIFA: .. 30 L. MWELEKEO WA MAPATO: .. 32 Mapato ya Ndani .. 32 Mapato ya Nje .. 33 M. MWELEKEO WA MATUMIZI .. 34 N. UGATUZI WA MADARAKA .. 37 O. MAZINGATIO MAALUM YA SERIKALI .. 38 P. MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUIMARISHA MAPATO .. 44 Q. SURA YA BAJETI .. 49 R. SHUKRANI .. 55 S. HITIMISHO: .. 58 1 MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mbele ya Baraza lako hili tukufu mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya SERIKALI ya MAPINDUZI ya ZANZIBAR kwa mwaka wa fedha wa 2017/18.
3 Kwa kutekeleza azma hiyo, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako sasa likae kama Kamati Maalum ya kupokea na kujadili mapendekezo hayo. 2. Mheshimiwa Spika, imani inatutaka waumini kuanza kwa jina la Mwenyezi Mungu, Muumba wetu. Naomba nami nianze kwa kumtukuza na kumshukuru sana Mola wetu, Subhana, kwa neema zake anazoendelea kutujaalia ambazo miongoni mwake ndio zimetuwezesha sisi kuwepo hapa alasiri hii kutimiza wajibu wetu kwa jamii iliyotupa ridhaa ya kuiongoza na kusimamia maendeleo yake. Kwangu mimi pia, bila ya neema hizo za uhai, afya na utulivu wa kila namna alionijaalia Muumba wetu, nami nisingeweza kutekeleza wajibu huu.
4 Namshukuru na kumdhukuru sana mola wetu. 2 3. Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 105 cha Katiba yetu ya mwaka 1984, kama ilivyorekebishwa, kinamtaka WAZIRI mwenye dhamana ya fedha kutayarisha na kuwasilisha mbele ya Baraza lako hili makadirio ya matumizi ya SERIKALI kwa mwaka unaofuatia. Kwa kuwa mwaka wa fedha mpya wa 2017/18 unakaribia kuanza, nakushukuru Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ya kutimiza wajibu wangu wa Kikatiba kwa dhamana yangu ya Uwaziri wa Fedha na Mipango. 4. Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26 cha Katiba yetu kinaweka dhima ya uongozi wa nchi yetu.
5 Kifungu ndicho kinaweka uwepo wa Rais wetu, kinampa dhamana ya kuwa ndie Mkuu wa nchi yetu ya ZANZIBAR , kuwa Kiongozi Mkuu wa SERIKALI ya MAPINDUZI na pia kuwa Mwenyekiti wa Baraza la MAPINDUZI . Kiongozi huyu anapatikana kwa njia ya uchaguzi unaofanywa na wananchi wenye sifa za kuchagua. Kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka jana (2016), kwa sasa Rais wetu, Mkuu wa nchi ya ZANZIBAR , Kiongozi Mkuu wa SERIKALI ya MAPINDUZI ya ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza letu la MAPINDUZI ni Dkt. Ali Mohamed Shein. Ndie aliyechaguliwa na Wananchi walio wengi kuwaongoza kwa miaka mitano hii.
6 3 5. Mheshimiwa Spika, Sisi sote ni mashahidi wa uongozi thabiti, wenye subra, hekima na uadilifu mkubwa wa Mhe. Dkt. Shein. Tumeshuhudia mwaka mwengine wa mafanikio ya pekee chini ya uongozi wake. Naomba tu uniruhusu, kwa sasa, nitumie fursa hii kumpongeza sana Mhe. Dkt. Shein kwa uongozi mahiri na kumaliza vyema mwaka mmoja wa kipindi cha pili cha uongozi wake. Kwangu mimi sina budi pia kumshukuru sana kwa imani yake inayoendelea kwangu inayodhihirika katika uamuzi wake wa kuendelea kunipa dhamana kubwa ya kuiongoza Wizara hii roho ya SERIKALI , Wizara ya Fedha na Mipango.
7 Kwa dhati ya nafsi yangu namuombea Mheshimiwa Rais kuendelea kuwa mfano wa uongozi wa uadilifu, uongozi uliojaa hekima na uongozi wa kuwapenda bila ya ukomo watu wote anaowaongoza. 6. Mheshimiwa Spika, mafanikio tunayoyaona kwa Mhe. Rais yanachangiwa pia na ushauri na usaidizi mzuri kutoka kwa msaidizi wake wa karibu, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais na kiongozi wa shughuli za SERIKALI hapa Barazani. Mhe. Balozi Seif nae amejipambanua kwa uongozi imara, usioyumba na usaidizi wa dhati kwa Rasi wetu. Nasi tunampongeza sana na kumshukuru kwa miongozo yake 4 anayotupatia katika kuhakikisha uwepo wa utendaji ulio bora.
8 7. Mheshimiwa Spika, niruhusu pia nitumie fursa hii kuwakaribisha na kuwapongeza sana mwenzetu, Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya na Mheshimiwa Ahmada Yahya Abdulwakil ambao wameteuliwa na Mheshimiwa Rais, kuwa Wajumbe wa Baraza hili muhimu. Pili kwa Mheshimiwa Dr Sira kuwa Mjumbe wa Baraza la MAPINDUZI na hivyo WAZIRI asiye na Wizara Maalum. Namkaribisha tena Dr Sira nikijua kuwa sio mgeni katika Baraza hili na nikitambua mchango wake mkubwa katika Baraza lililopita. Tunawaombea kwa Allah Mtukufu utumishi shupavu na imara kwa wananchi wote. 8. Mheshimiwa Spika, Baraza letu hili limeonesha utendaji imara wa kuisimamia SERIKALI .
9 Mwaka mmoja wa uhai wa Baraza hili la tisa umeweka viwango vipya vya utendaji wa chombo hiki muhimu kwa uhai na maendeleo ya ZANZIBAR . Nachukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Naibu wako Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma, Wenyeviti wa Baraza, Mheshimiwa Shehe Hamad Mattar na Mheshimiwa Mwanaasha Khamis 5 Juma na Wajumbe wote wa Baraza hili. Utendaji wa mwaka huu mmoja umedhihirisha kuwa tukishirikiana vyema, kwa umoja wetu tuna nafasi kubwa ya kuwatumikia vyema Wananchi wote wa ZANZIBAR .
10 9. Mheshimiwa Spika, umoja wetu huo unadhihirika tena katika kikao hiki cha Bajeti kwa Waheshimiwa Wajumbe kuisimamia vyema SERIKALI , kuihoji na kuwakilisha maslahi ya Wananchi wa Majimbo wanaowawakilisha bila ya kusahau maslahi makubwa zaidi ya Taifa. Hongereni sana Waheshimiwa Wajumbe wote. 10. Mheshimiwa Spika, Katiba yetu, chini ya Kifungu cha 9, imeweka bayana kuwa mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe. Kwamba nguvu na uwezo wa SERIKALI kufuatana na Katiba unatoka kwa wananchi wenyewe. Ni dhahiri kuwa, pamoja na kutoa ridhaa yao kwa Chama na viongozi wa kuwaongoza, wananchi ndio wenye mamlaka ya kuongoza nchi na hivyo wana nafasi muhimu sana katika utawala na maendeleo yao.