Example: air traffic controller

KIKUNDI CHA YES WE CAN SOCIAL CLUB (YCSC) …

KIKUNDI CHA YES WE CAN SOCIAL CLUB. (YCSC). KATIBA. YA. KIKUNDI . (YCSC). FOUTH DRAFT. YALIYOMO. 1. SEHEMU YA KWANZA ..4. TAARIFA YA KIKUNDI :.. 4. UFAFANUZI WA MANENO: .. 4. 2. SEHEMU YA MADHUMINI YA KIKUNDI : .. 5. 3. SEHEMU YA TATU ..5. UANAKIKUNDI .. 5. Sifa za kuwa Mwanakikundi .. 5. Haki za Mwanakikundi .. 6. Wajibu wa Mwanakikundi kwa KIKUNDI .. 6. Maadili ya 7. Ukomo wa 7. 4. SEHEMU YA NNE ..8. Michango .. 8. Mchango wa 8. Michango (Ada) ya kila mwezi .. 8. Michango Mingine .. 8. Faini (Penalty) na Adhabu Nyingine .. 8. Kuhifadhi Fedha na Akiba za 9. 5. SEHEMU YA TANO .. 10. Vyanzo vya Fedha .. 10. 6. SEHEMU YA SITA .. 11. Mikutano ya KIKUNDI .. 11. Mkutano Mkuu wa Wanakikundi .. 11. Mkutano wa Kawaida wa kila mwezi .. 11. Mkutano Mkuu wa Dharura .. 11. Mkutano Maalum wa Uchaguzi .. 11. Utoaji wa Taarifa za Mikutano au Vikao.

2. SEHEMU YA PILI 2.1 DHUMUNI KUU KIKUNDI a. Kushirikiana kijamii na kiuchumi Malengo mahususi: (a) Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha.nk

Information

Domain:

Source:

Link to this page:

Please notify us if you found a problem with this document:

Other abuse

Transcription of KIKUNDI CHA YES WE CAN SOCIAL CLUB (YCSC) …

1 KIKUNDI CHA YES WE CAN SOCIAL CLUB. (YCSC). KATIBA. YA. KIKUNDI . (YCSC). FOUTH DRAFT. YALIYOMO. 1. SEHEMU YA KWANZA ..4. TAARIFA YA KIKUNDI :.. 4. UFAFANUZI WA MANENO: .. 4. 2. SEHEMU YA MADHUMINI YA KIKUNDI : .. 5. 3. SEHEMU YA TATU ..5. UANAKIKUNDI .. 5. Sifa za kuwa Mwanakikundi .. 5. Haki za Mwanakikundi .. 6. Wajibu wa Mwanakikundi kwa KIKUNDI .. 6. Maadili ya 7. Ukomo wa 7. 4. SEHEMU YA NNE ..8. Michango .. 8. Mchango wa 8. Michango (Ada) ya kila mwezi .. 8. Michango Mingine .. 8. Faini (Penalty) na Adhabu Nyingine .. 8. Kuhifadhi Fedha na Akiba za 9. 5. SEHEMU YA TANO .. 10. Vyanzo vya Fedha .. 10. 6. SEHEMU YA SITA .. 11. Mikutano ya KIKUNDI .. 11. Mkutano Mkuu wa Wanakikundi .. 11. Mkutano wa Kawaida wa kila mwezi .. 11. Mkutano Mkuu wa Dharura .. 11. Mkutano Maalum wa Uchaguzi .. 11. Utoaji wa Taarifa za Mikutano au Vikao.

2 12. Uongozi wa KIKUNDI .. 12. Mfumo wa Uongozi (Kamati Kuu) ya KIKUNDI .. 12. Wajibu na kazi za viongozi wa KIKUNDI .. 12. Muda wa Uongozi wa KIKUNDI .. 13. Kusitishwa kwa Uongozi .. 13. 7. SEHEMU YA SABA .. 14. Kamati za KIKUNDI .. 14. Kamati 14. Kamati ya Nidhamu na Maadili .. 14. Kamati ya Fedha na Mikopo .. 14. 8. SEHEMU YA 16. Utaratibu wa Kutoa Maoni/Mapendekezo .. 16. Utatuaji wa Migogoro au Malalamiko .. 16. Mialiko ya KIKUNDI .. 16. Marekebisho/ Mabadiliko ya Katiba .. 16. 9. SEHEMU YA TISA .. 17. Kufutwa kwa KIKUNDI .. 17. Kuthibitishwa na Kusainiwa .. 17. 1. SEHEMU YA KWANZA. TAARIFA YA KIKUNDI : (a) Jina la KIKUNDI litakuwa: YCSC (YES WE CAN SOCIAL CLUB). yaani KIKUNDI kamili kwa watu waishio ndani ya Tanzania (b) Anuani ya KIKUNDI : 0000 Dar es salaam (c) Tarehe ya kuandikishwa: .. (d) Nambari ya kuandikishwa.

3 (e) Wanakikundi waanzilishi: .. (f) Eneo la shughuli za KIKUNDI litakuwa: Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (g) Makao makuu ya KIKUNDI yatakuwa: Dar es salaam (h) Lugha rasmi ya kuendesha shughuli za KIKUNDI itakuwa: Kiswahili au Kiingereza UFAFANUZI WA MANENO: Maneno yafuatayo yanapotumika katika masharti haya yatakuwa na maana kama inavyoelezwa hapa chini:- (a) KIKUNDI lina maana ya KIKUNDI cha YES WE CAN SOCIAL CLUB. (b) Mwanakikundi ni mtu yeyote aliyejiunga na KIKUNDI na anayeshiriki kikamilifu kutimiza kanuni na taratibu za KIKUNDI . (c) Viongozi ni wanakikundi waliochaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa katiba hii au kanuni za KIKUNDI , kusimamia mali au uendeshaji wa shughuli yoyote ya KIKUNDI . (d) Mtoto ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18. (e) Kitega uchumi (Investment) ni uwekezaji wenye kuleta tija kwa KIKUNDI (f) Kanuni za KIKUNDI ni taratibu zote zilizopitishwa na wanakikundi kutumika kwenye KIKUNDI katika kuitekeleza katiba hii na kufanikisha madhumuni/malengo ya KIKUNDI .

4 (g) Ndani ya Tanzainia Ndani ya nchi ni mipaka ambayo kijiografia inahusisha maeneo yote ndani ya jamhuri ya muungana na nje ya nchi itamaanisha maeneo yote yasiyokuwa ya Tanzania (h) Mkutano halali ni kikao chochote au mkutano wowote wa wanachama ulioitishwa kulingana na katiba hii au kanuni za KIKUNDI na uliofanywa kwa utaratibu uliowekwa. 2. SEHEMU YA PILI. DHUMUNI KUU KIKUNDI . a. Kushirikiana kijamii na kiuchumi Malengo mahususi: (a) Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na (b) Kuwezesha wanakikundi kuimarishana kiuchumi na hali ya maisha kwa:- i. Kupokea na kuweka michango ya fedha za wanakikundi ii. Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote halali za kiuchumi kwa manufaa ya wanakikundi kama itakavyokubaliwa katika mkutano halali wa wanakikundi iii. Kuwezesha kifedha shughuli binafsi za wanakikundi kwa masharti yaliyokubaliwa na wanakikundi iv.

5 Kuhamasisha ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama ulemavu, uzee, uyatima, uathirika wa ukimwi na watoto wa mitaani. 3. SEHEMU YA TATU. UANAKIKUNDI. Sifa za kuwa Mwanakikundi (a) Awe raia wa Tanzania. (b) Awe ni mtu mwenye akili timamu na wa kuaminika. (c) Awe anayefanya kazi iliyo rasmi ama isiyo rasmi au shughuli zinazokubalika kisheria (d) Awe ametimiza umri wa miaka 18. (e) Awe ni mtu aliye tayari kuiheshimu, kuitetea na kuongozwa kwa katiba ya KIKUNDI na kanuni zake (f) Awe ametimiza taratibu zote za kujiunga na KIKUNDI : i. Kujaza fomu ya maombi na kukubaliwa na uongozi kisha kupitishwa na mkutano mkuu kuwa mwanachama. ii. Kulipa kiingilio kama inavyoonyeshwa katika kanuni za KIKUNDI , au kama itakavyo amuliwa na Mkutano halali wa KIKUNDI . iii. Ili kuondoa tofauti ya michango kati ya mwanakikundi ambaye yupo na yule anayetaka kujiunga, wanakikundi watakubaliana kiasi cha fedha atakachotakiwa kuchangia mtu anayetaka kijiunga na muda wa kukamilisha mchango huo.

6 Haki za Mwanakikundi Mwanakikundi atakuwa na haki zifuatazo:- 1. Kutumia na kupata huduma zote za KIKUNDI bila ubaguzi. 2. Kupokea taarifa za KIKUNDI , kuona taarifa au kumbukumbu za KIKUNDI kwa utaratibu unaokubalika 3. Kuchagua (yaani kupiga kura) na kuchaguliwa (yaani kupigiwa kura) kwenye nafasi yoyote katika KIKUNDI 4. Haki ya kura moja kwa kila mwanakikundi bila kujali kiasi cha michango aliyoweka kwenye KIKUNDI . 5. Haki ya kujitetea dhidi ya jambo lolote litakalomkabili katika uhusiano wake na wanakikundi wengine. 6. Haki ya kutoa hoja yoyote inayohusu mwenendo wa wanakikundi ndani ya mikutano ya KIKUNDI 7. Haki ya kujitoa kwa hiari kwenye KIKUNDI 8. Mwanakikundi ambaye uanakikundi wake umekoma kwa sababu zilizoanishwa katika kifungu hapo chini, atarudishiwa fedha zake kulingana na mgawanyo wa thamani za KIKUNDI kwa wakati huo kwa wanachama wote ndani ya siku tisini (90) baada ya KIKUNDI kupata taarifa ya maandishi kwa kuzingatia yafuatayo:- i.

7 Marejesho yatafanyika baada ya kuzingatia matumizi (pamoja na hasara) ya KIKUNDI yaliyotokea kwa kipindi chote alichokuwa mwanakikundi ii. Mwanakikundi hatarejeshewa fedha zake mpaka madeni yake na ya wanakikundi wote aliowadhamini yawe yamelipwa yote au kupata mdhamini mwingine. iii. Asilimia ishirini (20%) ya kiasi kilichobaki baada ya kipengele (i) na (ii) hapo juu kutumika, itabaki kwenye mfuko wa KIKUNDI . Kiasi hiki kitatumika kadiri ya kanuni za KIKUNDI kwa maendeleo ya KIKUNDI . iv. Wajibu wa Mwanakikundi kwa KIKUNDI Mwanakikundi atakuwa na wajibu ufuatao kwa KIKUNDI :- 1. Kuchangia fedha kila mwezi (ada) na michango mingine yoyote kama itakavyoanishwa kwenye kanuni au iliyopendekezwa na kuidhinishwa na wanakikundi 2. Kuhudhuria na kushiriki katika mikutano yote halali ya KIKUNDI . 3. Kuwa mtu Mwaminifu, Mwaadilifu, na Mwenye Kujitolea kwa ajili ya KIKUNDI 4.

8 Kufuata kanuni, sheria na masharti ya KIKUNDI yaliyo kubaliwa 5. Kutii na kufuata maazimio yote ya Mkutano wowote halali hata ikiwa hakuwepo kwenye mkutano huo, au kutoshiriki katika kupitisha azimio hilo 6. Kueneza sifa nzuri za KIKUNDI 7. Kuwa na nidhamu wakati wa vikao au mkutano 8. Kushiriki kikamilifu kubuni miradi ya kuendeleza na kuimarisha KIKUNDI 9. Kutunza siri zote za KIKUNDI Maadili ya Mwanakikundi Kila mwanakikundi atapaswa kufuata maadili yafuatayo: (a) Kupendana na kuheshimiana (b) Kukubali kukosolewa endapo maadili yamekiukwa (c) Mwanakikundi haruhusiwi kupokea wala kutoa rushwa (d) Kuepuka dharau, kiburi, chuki na hasira (e) Kutoshiriki mikutano yoyote itakayofanyika kinyume na katiba na kanuni za KIKUNDI (f) Mwanakikundi anapokwenda kinyume na maadili ya KIKUNDI ataonywa mara ya kwanza kwa mdomo, tatu kwa maandishi na Kamati tendaji.

9 Asipobadilika kipengele cha kumwachisha uwanakikundi kitatumika Ukomo wa Uanakikundi (a) Kifo (b) Kushindwa kuchangia michango ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3) mfululizo kwa sababu zozote zile bila taarifa ya mdomo au kwa maandishi (c) Mwanakikundi kujiuzulu au kuomba kuacha uanakikundi yeye mwenyewe kwa sababu zozote zile (d) Kutoa au kupokea rushwa kwa viongozi au mwanakikundi yeyote (e) Kuachishwa uanakikundi kwa azimio litakaloungwa mkono na Wanakikundi wasiopungua theluthi mbili (2/3) ya Wanakikundi waliohudhuria katika Mkutano halali (f) Kushiriki katika kuiba au kuhujumu mali za KIKUNDI (ikiwa ni pamoja na fedha). (g) Mtu aliyeacha au kufukuzwa uanakikundi anaweza kuomba kujiunga tena kwa mujibu wa masharti ya uanakikundi kama yalivyo lakini atatakiwa kuwa na wadhamini wawili (2) ambao ni wanakikundi hai.

10 (h) Mwanakikundi anaweza kurithisha uanakikundi kwa wale wanaomtegemea; na yule anayerithishwa kama inavyoonyesha kwenye fomu na awe na sifa zilizoanishwa katika kifungu namba 4. SEHEMU YA NNE. Michango Mchango wa Kiingilio (a) Mwanakikundi mwanzilishi anawajibika kulipa kiingilio cha shilingi laki moja (Tshs 100,000) kabla ya tarehe 31/01/2015. (b) Mwanakikundi atakeyejiunga baada ya tarehe 31/01/2015 hatakuwa mwanzilishi na atatakiwa kulipa mchango kulingana na kanuni za KIKUNDI . (b) Mtu aliyejiunga na KIKUNDI atastahili haki za Mwanakikundi pale atakapokuwa amelipa mchango wa kiingilio. (c) Kila atakayejiunga na KIKUNDI atapatiwa fomu ya usajili ambayo itaonyesha kiasi anachotakiwa kulipa kuwa Mwanakikundi, kiasi alicholipa na utaratibu wa kukamilisha kiasi kilichobaki. Michango (Ada) ya kila mwezi (a) Mwanakikundi atatakiwa kulipa kwa wakati kiasi kilichopitishwa kama ada ya kila mwezi kama ilivyoainishwa katika kanuni na taratibu za KIKUNDI .


Related search queries